UANZILISHI
WA FAMILIA NA MTANDAO WA VIJANA,
JIJI
LA MBEYA NA MAENEO JIRANI KUFUATIA UPATIKANAJI WA VIJANA WAHUSIKA
MTANDAO
UNAOZINGATIA UMRI, KIPAJI, UJUZI ELIMU NA MAHITAJI YA JAMII
MTANDAO
WA ASILI YETU , MTANDAO UTAOJULIKANA KWA JINA LA “YETU NETWORK ORGANIZATION”
“ ASILI YETU FOUNDATION”
TAFADHARI
HUSIKA.
Ndugu
Kijana na mshiriki wa maisha ya karne hii ya 21 Ijulikanayo kama karne ya
sayansi na Teknolojia Ikiwa ni tafsiri halisi na sahihi katika maana ya Kizazi
cha Ishirini na’"" tena tukikawia sema hivo basi Tunalazimika kuzungumza ya kuwa
“kizazi Tegemewa kwa Maendeleo ya jamii” na ufanisi katika ulimwengu huu wa
sasa. Kwa pamoja na kwa ushirikiano wenye adhma adimu ya Kuijenga jamii hii kwa
kuongozwa na msamiati huu
“Ukipata
nafasi ya kuishi katika ulimwengu huu, jitahidi Kuondoka na kuuacha ulimwengu
huu ukiwa Bora tofauti na ulivo Ukuta”
Tunamaanisha
kwa lugha ya kigeni “when you get a chance to live in this world makes sure you leave it better
than the way you have Found it”
Hivo
ni dhahili ya kuwa kama tutasahau ya kuwa Muda ndio huu, bas ni lazima kwa
pamoja Tuungane na kuamini ya kuwa wakati huo ni Sasa. Tena leo.
Hii
ni katika maana halisi ya kuwa tutatumia fursa na ujuzi, uzoefu katika harakati
ya maisha, Taaluma tuliyopewa darasani, na kuamini ya kuwa Tunawenada kuuacha
ulimwengu huu ukiwa bora zaidi ya Tulivoukuta.
Ndugu
Mhusika, Imejulikana ya kuwa Ukitaka fika haraka katika safari yako Nenda peke
yako, lakini ukitaka Fika Mbali ni budi Kwenda Pamoja.
Jamii
ni sisi na usisi huu ni maana ya tafsiri ya pamoja. Hivo basi ili tufike mbali
ni lazima Tuondoke pamoja na Kufika Mbali.
Ndugu,
Kama wanadamu tumeumbwa na Maono yenye kutambua jema na baya tena Zuri na enye
Karaha hivo tunajua Ugumu na wepesi wa ufanisi wa kila jambo tena tuambatanayo
katika Maisha ya kila siku, ambapo Hii inajulikana kama “maisha ni jumla ya
matotokeo ya ufanyacho
” Hivo basi Kila wepesi una ugumu upelekeao matokeo ya tufanyacho Na ni tafsiri ya kani tutumiayo kufanikisha Hayo.
” Hivo basi Kila wepesi una ugumu upelekeao matokeo ya tufanyacho Na ni tafsiri ya kani tutumiayo kufanikisha Hayo.
Hivo
basi ni dhahiri kila mmoja atatambua ya kuwa mara zote ugumu wa ufanikishi wa
jambo ni baada ya kuwa na kani ndogo katika ufanikishi, Hii inamaana ya ukuwa
Umoja ni dhaifu daima na Muungano ni Imara daima. Hivo basi ili kufanikisha
urahisi wa ufanisi na ufanikishaji wa mipango mikakati ya Kujenga jamii bora Ni
budi Kuungana.
Kama
vijana Tunakuja na adhma moja ya kuungana na Kuunda matandao wa pamoja amabao
utatuunganisha na kutokomeza tofauti mbalimbali za rika, jinsia, uwezo, taaluma
na Eneo la Upatikanaji, Hii ni adhma ambayo inatuunganisha vijana wote , Jinsia
zoote na Rika tofauti katika Kutimiza Mpango mkakati wa kujenga Jamii bora
zaidi.
Hivo
basi kwa mara ya Kwanza na kwa ushiriki shirikishi Tunaamini ya kuwa ni muda wa
MIMI na WEWE leo hii kufanikisha hili.
Hivo
naomba tuweke wazi mambo yafuatayo katika mwenendo wa Mtandao huu.
1.
Kwa
kuwa asili ya kila mmoja wetu yaani mimi na wewe ni katika FAMILIA, ianatupasa
kuanza kuunda ushiriki wetu katika maudhui ya FAMILIA. Hii inamaanisha ya kuwa
mtandao wetu utaunda muungano wa kila mmoja mbele na nyuma yetu kufanikisha
ushiriki na utatuzi wa changamoto na mambo yoote yanayotuhusu katika nafasi ya
FAMILIA. Jema na Karaha litatatuliwa kwa nguvu ya pamoja.
2.
Kuwa
na maisha ya familia inamaana ya kuwa pamoja kwa kila jambo kwa umbali na
ukaribu wa kila mmoja wetu aliye ndani ya mtandao huu. Hivo ni jukumu la kila
mmoja wetu yaani mimi na wewe Kumsogeza kila aliye karibu nawe kuwa ndani ya
mtandao huu ili kuleta maana ya Kuwa wamoja.
3.
Mtandao
unamaana ya kushirikiana kwa pamoja katika dhana ya familia ili lolote lihusulo
nafasi ya familia tuwe wamoja.
4.
Mtandao
huu utakuawa katika utekelezaji wa jukumu la awali litakaloitwa “Njoo wewe na
waje Woote” yaani “come one Welcome All” ambapo ndipo inapoanzia familia na
mtandao kwa ujumla. Na ndio jukumu lililopo kwa sasa nan i jukumu la mimi na
wewe kwa sasa kuhakikisha ya kuwa kila rafiki aliye karibu na mbali yako
anakuawa mwana mtandao huu ili kufanikisha adhma hii. Hili halizingatii tofauti
yoyote iliyopo baina yetu.
5.
Tunakuwa
ndani ya mtandao wa watu wenye Umri tofauti, elimu tofauti, vipaji tofauti, na
uchumi tofauti, hivo ili usawa uwepo ndani ya haya ni lazima tukubali kuwa
wamoja na wenye USHIRIKI wa pamoja.
6.
Baada
ya kuwa na familia ya pamoja tunaimani na kuwa Hatuwezi kukaa na kusubiri faraja
au matatizo Yatokee. Ndipo tuoneshe ufanisi wetu. Ni lazima ifike hatua tuamini
ya kuwa tunatumia uzoefu wa harakati za maisha, Taaluma tulizo nazo, Na vipaji
vyetu kujijenga sisi na Jamii kwa ujumla. Hili ni katika kutimiza adhma ya
kuajiajili katika fursa endelevu za kujenga jamii.
7.
Mtandao
wetu utalazimika kujigeuza kuwa Taasisi ya vijana ambao utajulikana kama ASILI YETU. ambapo ikiwa hilo ni jina la awali wanamtandao watapendekeza jina
madhubuti lenye Muungano wa pamoja.
8.
Mtandao
utapitisha logo ya kutambulisha mtandao na kupendekeza kanuni na taratibu za
kutumika katika Taasisi
9.
Kuwa
na Uongozi wa Mtandao na kuweka misingi ya uratibu wa mtandao na kamati za
utendaji ndani yake ambao ndipo tutapojenga muungano kati ya Mtandao na Familia
na kuratibu muendelezo wa Muungano wetu.
10. Kujitangaza katika jamii na kushiriki
katika shughuri za kujenga jamii bora. Ambapo tunataraji kuwa na walezi watakao
tujenga kimawazo na Kujenga ushiriki ndani yetu.
11. Walezi watakuawa ndio kamati na ushauri
na uhakikin wa mipango mikakati na kuwa waratibu wa vikao na majadiliano,
kufanikisha mwendelezo na uhai wa Familia.
12. Ufanikishaji wa mikakati itakayo enda
kwa jina la Miradi itakayokuwa endelevu kwa uhai wa familia na taasisi.
13. Ushiriki wa kila mmoja kwa nafasi na
ujuzi alionao kwa kuzingatia uwepo wake ndani ya familia huku tukiamini ya kuwa
kila nafasi ya aliyendani yetu ni ya muhimu na adimu.
14. Kuandaa na kuwa na wadhamini ndani ya
taasisi mkabala na walezi ambao watakuwa
na nafasi ya kushiriki nasi katika mafanikio na ufanikishaji ya kila jambo
15. Baada ya kuwa na familia kama ilivokuwa
dhima ya umoja huu naamini na taasisi itakuwa tayari imeanza na kuwa ndio
mhimili wa kudumu wa muungano na mtandao wetu, hivo ni budi kuwa na mipango
mikakati ya kufanya ili kuwa na maadhimisho ya jambo kila baada ya muda Fulani
kama itavopendekezwa na wanamtandao na piah kuwa na UTAYARI wa kujipambanua kwa kuongeza idadi ya
wanachama na Wanamtandao kwa ujumla ili kuweza fikia lengo la kujenga jamii
bora tofauti na tulivoikuta.
IKIWA KAMA NI NAFASI.
Basi
familia na mtandao kwa ujumla tunaamini ya kuwa nifursa pekee ya kuunda mkakati
endelevu wa kusaidia jamii na sisi ndani yetu ambapo utekelezaji wa haya yote
ni pale itapofika Hitma yake, Na mwendelezo ramsi utaanza pale
itapofikia usajili wa kudumu.
ASILI YETU inatarajia kuongoza harakati za kujikomboa kama vijana
katika fursa mbalimbali za maisha ambapo taswira iliyopo juu ya umaskini ,
maradhi na Ujinga iwe sababu ya kupambana na Nyenzo zote kandamizi katika
kupambanua maendeleo ya kijana na jamii yake. Tunatarajia kwa pamoja kufungua
maono ya ushiriki kwa kutozingatia
jinsia bali kwa kila jambo linalogusa na kugonga jamii.
Tutasaidiana
kwa pamoja kufungua fursa na uwezo ndani yetu kwa hurka ya maendeleo zaidi
Tutakuwa
na makundi mbalimbali ya ufanisi tukilenga katika Nyanja kubwa kama ifuatavyo.
1.
Elimu
2.
Teknolojia
3.
Uchumi
na biashara
4.
Kilimo
5.
Utawala,
sharia na siasa
6.
Takwimu
na mipango
7.
Mipango
na utafiti
KUHUSU WEWE.
Tunaamini na kukiri ya kuwa uwepo wako ndani ya familia na
taasisi yetu utadfanikisha yafuatayo.
·
Kuleta
matokeo makubwa na mafanikio kusudiwa.
·
Kushirikiana
kwa pamoja na kufanya ujumla wa ushiriki wa wote na kuwa tayari kuwashirikisha
wengine katika kila jambo ambalo linahusu familia na mtandao pamoja.
·
Kuwa
tayari kujifunza na kufundisha wengine kwa kile ulichonancho.
Hili litafikiwa
baada ya kuwa tayari kujitoa kuwajibika, kuwashirikisha wengine na Kupatikana
kwa kila jambo ambalo litahusu Mtandao wetu.
YAHITAJIKAYO.
·
Hamu
na njaa ya mabadiliko na utayari wa
maendeleo.
·
Ujuzi
binafsi, Elimu binafsi ya nafasi yoyote, na Kipaji cha tija haswa hitajika.
·
Uwajibikaji,
ushiriki, upatikanaji.
HITIMISHO.
Kwa
pamoaja na kwa Tija ya ushirikiano naomba soote tuwe karibu na kushirikiana ili
tufikie pamoja, naomba tushirikine katika mawazo, nguvu na nia moja kuanzia
hapa mpaka mwisho, kwani taswira halisi ya haya yote ni SISI. Mungu atubariki
na kutulinda Atupe nguvu na uvumilivu Wote. Akhsanteni.
Wenu:
ASILI YETU TEAM 2017.
kny: Timu ya Uratibu.