Wednesday 4 November 2015

TAARIFA YA MUHIMU KUTOKA IDARA YA URATIBU NA UFANIKISHAJI WA UUNDWAJI WA FAMILIA NA MTANDAO KWA PAMOJA.



UANZILISHI WA FAMILIA NA MTANDAO WA VIJANA,


JIJI LA MBEYA NA MAENEO JIRANI KUFUATIA UPATIKANAJI WA VIJANA WAHUSIKA


MTANDAO UNAOZINGATIA UMRI, KIPAJI, UJUZI ELIMU NA MAHITAJI YA JAMII


MTANDAO WA ASILI YETU , MTANDAO UTAOJULIKANA KWA JINA LA                                 “YETU NETWORK ORGANIZATION”

                                                              “ ASILI YETU FOUNDATION”
       TAFADHARI HUSIKA.

Ndugu Kijana na mshiriki wa maisha ya karne hii ya 21 Ijulikanayo kama karne ya sayansi na Teknolojia Ikiwa ni tafsiri halisi na sahihi katika maana ya Kizazi cha Ishirini na’"" tena tukikawia sema hivo basi Tunalazimika kuzungumza ya kuwa “kizazi Tegemewa kwa Maendeleo ya jamii” na ufanisi katika ulimwengu huu wa sasa. Kwa pamoja na kwa ushirikiano wenye adhma adimu ya Kuijenga jamii hii kwa kuongozwa na msamiati huu

“Ukipata nafasi ya kuishi katika ulimwengu huu, jitahidi Kuondoka na kuuacha ulimwengu huu ukiwa Bora tofauti na ulivo Ukuta”
Tunamaanisha  kwa lugha ya kigeni “when you get a chance to live in this world makes sure you leave it better than the way you have Found it”

Hivo ni dhahili ya kuwa kama tutasahau ya kuwa Muda ndio huu, bas ni lazima kwa pamoja Tuungane na kuamini ya kuwa wakati huo ni Sasa. Tena leo.
Hii ni katika maana halisi ya kuwa tutatumia fursa na ujuzi, uzoefu katika harakati ya maisha, Taaluma tuliyopewa darasani, na kuamini ya kuwa Tunawenada kuuacha ulimwengu huu ukiwa bora zaidi ya Tulivoukuta.

Ndugu Mhusika, Imejulikana ya kuwa Ukitaka fika haraka katika safari yako Nenda peke yako, lakini ukitaka Fika Mbali ni budi Kwenda Pamoja. 
Jamii ni sisi na usisi huu ni maana ya tafsiri ya pamoja. Hivo basi ili tufike mbali ni lazima Tuondoke pamoja na Kufika Mbali.

Ndugu, Kama wanadamu tumeumbwa na Maono yenye kutambua jema na baya tena Zuri na enye Karaha hivo tunajua Ugumu na wepesi wa ufanisi wa kila jambo tena tuambatanayo katika Maisha ya kila siku, ambapo Hii inajulikana kama “maisha ni jumla ya matotokeo ya ufanyacho
” Hivo basi Kila wepesi una ugumu upelekeao matokeo ya tufanyacho Na ni tafsiri ya kani tutumiayo kufanikisha Hayo. 
Hivo basi ni dhahiri kila mmoja atatambua ya kuwa mara zote ugumu wa ufanikishi wa jambo ni baada ya kuwa na kani ndogo katika ufanikishi, Hii inamaana ya ukuwa Umoja ni dhaifu daima na Muungano ni Imara daima. Hivo basi ili kufanikisha urahisi wa ufanisi na ufanikishaji wa mipango mikakati ya Kujenga jamii bora Ni budi Kuungana.

Kama vijana Tunakuja na adhma moja ya kuungana na Kuunda matandao wa pamoja amabao utatuunganisha na kutokomeza tofauti mbalimbali za rika, jinsia, uwezo, taaluma na Eneo la Upatikanaji, Hii ni adhma ambayo inatuunganisha vijana wote , Jinsia zoote na Rika tofauti katika Kutimiza Mpango mkakati wa kujenga Jamii bora zaidi.
Hivo basi kwa mara ya Kwanza na kwa ushiriki shirikishi Tunaamini ya kuwa ni muda wa MIMI na WEWE leo hii kufanikisha hili.

Hivo naomba tuweke wazi mambo yafuatayo katika mwenendo wa Mtandao huu.
1.      Kwa kuwa asili ya kila mmoja wetu yaani mimi na wewe ni katika FAMILIA, ianatupasa kuanza kuunda ushiriki wetu katika maudhui ya FAMILIA. Hii inamaanisha ya kuwa mtandao wetu utaunda muungano wa kila mmoja mbele na nyuma yetu kufanikisha ushiriki na utatuzi wa changamoto na mambo yoote yanayotuhusu katika nafasi ya FAMILIA. Jema na Karaha litatatuliwa kwa nguvu ya pamoja.

2.      Kuwa na maisha ya familia inamaana ya kuwa pamoja kwa kila jambo kwa umbali na ukaribu wa kila mmoja wetu aliye ndani ya mtandao huu. Hivo ni jukumu la kila mmoja wetu yaani mimi na wewe Kumsogeza kila aliye karibu nawe kuwa ndani ya mtandao huu ili kuleta maana ya Kuwa wamoja.

3.      Mtandao unamaana ya kushirikiana kwa pamoja katika dhana ya familia ili lolote lihusulo nafasi ya familia tuwe wamoja.
4.      Mtandao huu utakuawa katika utekelezaji wa jukumu la awali litakaloitwa “Njoo wewe na waje Woote” yaani “come one Welcome All” ambapo ndipo inapoanzia familia na mtandao kwa ujumla. Na ndio jukumu lililopo kwa sasa nan i jukumu la mimi na wewe kwa sasa kuhakikisha ya kuwa kila rafiki aliye karibu na mbali yako anakuawa mwana mtandao huu ili kufanikisha adhma hii. Hili halizingatii tofauti yoyote iliyopo baina yetu.
5.      Tunakuwa ndani ya mtandao wa watu wenye Umri tofauti, elimu tofauti, vipaji tofauti, na uchumi tofauti, hivo ili usawa uwepo ndani ya haya ni lazima tukubali kuwa wamoja na wenye USHIRIKI wa pamoja.

6.      Baada ya kuwa na familia ya pamoja tunaimani na kuwa Hatuwezi kukaa na kusubiri faraja au matatizo Yatokee. Ndipo tuoneshe ufanisi wetu. Ni lazima ifike hatua tuamini ya kuwa tunatumia uzoefu wa harakati za maisha, Taaluma tulizo nazo, Na vipaji vyetu kujijenga sisi na Jamii kwa ujumla. Hili ni katika kutimiza adhma ya kuajiajili katika fursa endelevu za kujenga jamii.
7.      Mtandao wetu utalazimika kujigeuza kuwa Taasisi ya vijana ambao utajulikana kama ASILI YETU. ambapo ikiwa hilo ni jina la awali wanamtandao watapendekeza jina madhubuti lenye Muungano wa pamoja.

8.      Mtandao utapitisha logo ya kutambulisha mtandao na kupendekeza kanuni na taratibu za kutumika katika Taasisi
9.      Kuwa na Uongozi wa Mtandao na kuweka misingi ya uratibu wa mtandao na kamati za utendaji ndani yake ambao ndipo tutapojenga muungano kati ya Mtandao na Familia na kuratibu muendelezo wa Muungano wetu.

10.  Kujitangaza katika jamii na kushiriki katika shughuri za kujenga jamii bora. Ambapo tunataraji kuwa na walezi watakao tujenga kimawazo na Kujenga ushiriki ndani yetu.

11.  Walezi watakuawa ndio kamati na ushauri na uhakikin wa mipango mikakati na kuwa waratibu wa vikao na majadiliano, kufanikisha mwendelezo na uhai wa Familia.

12.  Ufanikishaji wa mikakati itakayo enda kwa jina la Miradi itakayokuwa endelevu kwa uhai wa familia na taasisi.

13.  Ushiriki wa kila mmoja kwa nafasi na ujuzi alionao kwa kuzingatia uwepo wake ndani ya familia huku tukiamini ya kuwa kila nafasi ya aliyendani yetu ni ya muhimu na adimu.

14.  Kuandaa na kuwa na wadhamini ndani ya taasisi mkabala na  walezi ambao watakuwa na nafasi ya kushiriki nasi katika mafanikio na ufanikishaji ya kila jambo

15.  Baada ya kuwa na familia kama ilivokuwa dhima ya umoja huu naamini na taasisi itakuwa tayari imeanza na kuwa ndio mhimili wa kudumu wa muungano na mtandao wetu, hivo ni budi kuwa na mipango mikakati ya kufanya ili kuwa na maadhimisho ya jambo kila baada ya muda Fulani kama itavopendekezwa na wanamtandao na piah kuwa na UTAYARI  wa kujipambanua kwa kuongeza idadi ya wanachama na Wanamtandao kwa ujumla ili kuweza fikia lengo la kujenga jamii bora tofauti na tulivoikuta.

IKIWA KAMA NI NAFASI.

Basi familia na mtandao kwa ujumla tunaamini ya kuwa nifursa pekee ya kuunda mkakati endelevu wa kusaidia jamii na sisi ndani yetu ambapo utekelezaji wa haya yote ni pale itapofika Hitma yake, Na mwendelezo ramsi utaanza pale itapofikia usajili wa kudumu.
ASILI YETU inatarajia kuongoza harakati za kujikomboa kama vijana katika fursa mbalimbali za maisha ambapo taswira iliyopo juu ya umaskini , maradhi na Ujinga iwe sababu ya kupambana na Nyenzo zote kandamizi katika kupambanua maendeleo ya kijana na jamii yake. Tunatarajia kwa pamoja kufungua maono ya ushiriki  kwa kutozingatia jinsia bali kwa kila jambo linalogusa na kugonga jamii.
Tutasaidiana kwa pamoja kufungua fursa na uwezo ndani yetu kwa hurka ya maendeleo zaidi
Tutakuwa na makundi mbalimbali ya ufanisi tukilenga katika Nyanja kubwa kama ifuatavyo.
1.      Elimu
2.      Teknolojia
3.      Uchumi na biashara
4.      Kilimo
5.      Utawala, sharia  na siasa
6.      Takwimu na mipango
7.      Mipango na utafiti

KUHUSU WEWE.

Tunaamini na kukiri ya kuwa uwepo wako ndani ya familia na taasisi yetu utadfanikisha yafuatayo.
·         Kuleta matokeo makubwa na mafanikio kusudiwa.
·         Kushirikiana kwa pamoja na kufanya ujumla wa ushiriki wa wote na kuwa tayari kuwashirikisha wengine katika kila jambo ambalo linahusu familia na mtandao  pamoja.
·         Kuwa tayari kujifunza na kufundisha wengine kwa kile ulichonancho.
Hili litafikiwa baada ya kuwa tayari kujitoa kuwajibika, kuwashirikisha wengine na Kupatikana kwa kila jambo ambalo litahusu Mtandao wetu.

YAHITAJIKAYO.

·         Hamu na njaa ya mabadiliko na utayari wa maendeleo.
·         Ujuzi binafsi, Elimu binafsi ya nafasi yoyote, na Kipaji cha tija haswa hitajika.
·         Uwajibikaji, ushiriki, upatikanaji.

HITIMISHO.

Kwa pamoaja na kwa Tija ya ushirikiano naomba soote tuwe karibu na kushirikiana ili tufikie pamoja, naomba tushirikine katika mawazo, nguvu na nia moja kuanzia hapa mpaka mwisho, kwani taswira halisi ya haya yote ni SISI. Mungu atubariki na kutulinda Atupe nguvu na uvumilivu Wote. Akhsanteni.

Wenu:
ASILI YETU TEAM 2017.
kny: Timu ya Uratibu.