ASILI
YETU – YETU FOUNDATION- 2017
KATIBA YA KIKUNDI – ASILI YETU
(YETU FOUNDATION)
KIKUNDI CHA VIJANA NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
MKOA WA MBEYA
2017
“Ulipo
Tupo”
KATIBA YA ASILI YETU – ASILI YETU FOUNDATION.
YALIYOMO:
Contents
SEHEMU YA I: UTANGULIZI
IBARA YA 1: JINA LA KATIBA, KAULI MBIU NA KUANZA KUTUMIKA
1.1 Katiba hii itajulikana KamaKATIBA YA ASILI YETU -2017.
1.2 Kauli mbiu ya Chama Cha Asili Yetu ni : Ulipo tupo
1.3. Katiba hii imepitishwa Kwa kauli moja na
wanachama katika Mkutano Mkuu.
IBARA YA 2: TAFSIRI YA MANENO
2.1 ASILI: Chanzo na halisia ya kilichopo na Kilichoundwa katika
miliki ya Mwana-Adam.
2.2YETU: Miliki (kilichoonekana na Kisichoonekana)katika mazingira Ya
Mwana-Adamu.
2.3 FOUNDATION: Tafsiri ya lugha ya Kiingereza yenye maana ASILI.
TAFSIRI ZAIDI
a.Kikundi” lina maana ya Kikundi cha ASILI
YETU (YETU FOUNDATION)
b. “Mwanakikundi” ni mtu
yeyote aliyejiunga na
kikundi na anayeshiriki
kikamilifu kutimiza kanuni na
taratibu za kikundi.
c.”Viongozi”ni wanakikundi
waliochaguliwa au kuteuliwa
kwa mujibu wa katiba
hii au kanuni za kikundi, kusimamia mali au uendeshaji wa shughuli
yoyote ya kikundi.
d.“Mtoto” ni mtu mwenye
umri chini ya miaka 18.
e. “Kitega
uchumi”(Investment)ni uwekezajiwenye kuleta tijakwa kikundi
f. “Kanuni” za
kikundi ni taratibu zote
zilizopitishwa na wanakikundi
kutumika kwenye kikundi katika
kuitekeleza katiba hii na kufanikisha madhumuni/malengo ya kikundi.
g. “Ndani ya
Tanzainia” Ndani ya
nchi ni mipakaambayo
kijiografia inahusisha maeneo
yote ndani ya jamhuri
ya muungana na nje
ya nchi
itamaanisha maeneo yote yasiyokuwa
ya Tanzania
h. “Mkutano halali”
ni kikao chochote
au mkutano wowote
wa wanachama
ulioitishwa kulingana
na katibahii au kanuni za kikundi na uliofanywa kwa utaratibi uliowekwa
2.4 AINA YA KIKUNDI
ASILI YETU ni Kikundi cha
Kijamii cha Kimaendeleo ya Kiuchumi (Community Based Organisation - CBO)
SEHEMU YA II: KATIBA, USAJILI, OFISI KUU NA ENEO LA UTENDAJI
IBARA YA 3: Katiba ya kikundi cha Vijana wenye lengo la kuleta
mabadiliko chanya katika fikra Na matendo yenye Kuakisi Uzalendo Nauhalisia.
IBARA YA 4: Jina la
Kikundi litakuwa ASILI YETUNa kita
tambulika KamaAY.
IBARA YA 5: Usajili: Kikundi hiki kitakuwa chini ya sheria na.337
ya mwaka 2002 Na kitakuwa Kikundi cha hiari.
IBARA
YA 6:Ofisi kuu ya kikundi itakuwa MBEYA,
Mbeya Mjini, kata Ya Iganzo/Isanga Mtaa wa AsiliKama ilivyoamuliwa na Mkutano
Mkuu wa Kikundi. Pia zinaweza kuanzishwa
ofisi ndogo za kikundi Kwa kadiri itakavyoonekana Na mkutano mkuu kuwa inafaa
kuwa Na ofisi hizo
IBARA YA 7: Eneo la Utendaji kazi litakuwa eneo lote la Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Hususani Mkoa wa Mbeya, Mbeya Mjini.
IBARA YA 8: Katiba hii
inatoa nafasi ya kuwa na kanuni za Maadili kwa wanakikundi na Viongozi.
SEHEMU YA III: DIRA, DHAMIRA NA MADHUMUNI
IBARA YA 9: Kauli Dira ya ASILI
YETU itakuwa: Kuwa Kikundi pekee cha Kusaidina, kuungana na kunufahisha
wanakikundi Na jamii yake.
IBARA YA 10: Kauli ya Damira: Kuanzisha Na kutunza misingi ya
ushiriki wa pamoja katika utendaji na uanzishwaji wa shughuli za manufaa ya
wanakikundi na jamii.
IBARA YA 11: Madhumuni ya Kikundi ya takuwa Kama ifuatavyo;
A: LENGO KUU
Kushirikiana kijamii Na kiuchumi
B: MALENGO
MAHUSUSI
(a) Kushirikiana na kusaidiana wakati wa shida na raha
(b) Kuwezesha wanakikundi kuimarishana kiuchumi na hali ya
maisha kwa:
-i. Kupokea na kuweka michango ya fedha za wanakikundi
ii.
Kuanzisha Na kuendeleza shughuli zozote halali za kiuchumi kwa manufaa ya wanakikundi
kama itakavyokubaliwa katika mkutano halali wa wanakikundi
iii. Kuwezesha
kifedha shughuli binafsi za wanakikundi kwa masharti yaliyokubaliwa na wanakikundi
iv. Kuhamasisha
ushirikiano na wanakikundi wenye changamoto mbalimbali kama ulemavu,
v. Kushirikiana
Na uongozi wa Serikali na Idara mbalimbali katika shughuli mbalimbali za
maendeleo ya Jamaii kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu.
vi. Kusaidia
wanakikundi wake Na jamii zao Kwa lengo la kustawisha na kuboresha maisha yao.
Vii. Kuanzisha Na
kushiriki shughuli za kiuchumi Kama vile miradi ya kimaendeleo ambayo
itasimamiwa Na wanakikundi.
viii. Kuanzisha na kushiriki kuboresha huduma za jamii
kama elimu, afya, mazingira ,Uchumi na Michezo.
ix. Kufanya shughuli nyingine
yoyote isiyopingana Na sheria ambayo Jamii na mkutano mkuu utaridhia kuwa
ifanyike.
SEHEMU YA IV: UANACHAMA, AINA ZA WANACHAMA NA KURUDISHIWA
UANACHAMA
IBARA YA 12:UANACHAMA
12.0.
Kutakuwa na aina mbili zifuatazo za uanachama ambazo ni;
12.1.
Mwanachama wa Kawaida
Ni mtu yeyote yule ambaye ametimiza
taratibu zote za kujiunga Na Kikundi au Umoja huu Kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni zake ikiwa ni pamoja na kulipa Ada na Michango stahiki.
12.2.
Mwanachama wa Kutunukiwa
Mwanachama wa
Kutunukiwa ni Mtu yeyote atakaetunukiwa uanachama kupitia maamuzi au azimio la
Mkutano Mkuu katika kuthamini Mchango uliotolewa na Mtu huyo ama atakaoendelea
kuutoa kwa kuleta maendeleo na ufanisi wa Malengo ya Kikundi au Umoja huu.
12.2.1 Sifa za kuwa Mwanachama
(i)
Awe na Umri usiopungua miaka 18.
(ii)
Awe mwenye nia na awe tayari kuwa
mwanachama
(iii)
Awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye
shughuli za kikundi
(iv)
Awe na akili timamu.
(v)
Awe tayari kutii na kufuata masharti
ambayo yameainishwa kwenye Katiba na Kanuni za kikundi
(vi)
Awe tayari kulipa kiingilio pamoja na
ada ya uanachama ya kila mwezi
12.3.1 Haki za Mwanachama
(i) Kutoa maoni yake
kwa uhuru
(ii) Kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi
yoyote ile ya Uongozi katika Kikundi au Umoja huu.
(iii)
Kuwasiliana Na
Uongozi/Viongozi ikiwa ni pamoja na kupokea na kutoa taarifa zinazohusu Kikundi
au Umoja huu.
(iv)
Kuhudhuria na/au
kuwakilisha katika jambo lolote lile linalohusu Kikundi au Umoja huu Kwa
kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(v) Kupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea pindi anapokabiliwa
na tuhuma zozote zile dhidi yake katika umoja huu.
(vi) Kutumia Mali za
Kikundi kwa kufuata utaratibu na Kanuni za Umoja huu.
(vii) Ana haki ya kutoa
hoja yake na kusikilizwa wakati wa kushiriki majadiliano kwenye vikao.
(viii)
Kufahamu mapato na
matumizi ya Kikundi kwa kutumia na kuzingatia Kanuni.
(ix)
Kusaidiwa linapomtokea
tatizo.
(x) Kusaidiwa kimawazo au
kiuchumi kulingana na hali itakavyo ruhusu.
12.3.2 Wajibu wa Mwanachama.
(i)
Kuilinda na kuitetea katiba hii wakati
wote.
(ii)
Kutekeleza majukumu atakayopewa na
viongozi au wanachama wenzake.
(iii)
Kushiriki katika shughuli zote za
kikundi kwa mujibu wa katiba hii ikiwa ni pamoja na vikao halali vya Umoja huu.
(iv)
Kulipa ada pamoja na michango mbalimbali
itakayo pitishwa na Kikundi au Umoja
huu.
(v)
Kueneza
sifa nzuri za Umoja huu.
(vi)
Kutii
na kufuata maagizo na maazimio ya Mkutano/Mikutano halali ya Umoja huu, hata
ikiwa hatakuwepo kwenye Mkutano huo, au hakushiriki katika kupitisha azimio
hilo.
(vii)
Kuwa na
nidhamu wakati wa Mikutano ama shuhuli nyingine zozote za Kikundi.
(viii)
Kutunza
siri zote za Umoja huu
12.3.3
Kujiunga na Kikundi.
i. Kujaza Fomu
ya maombi itakayotolewa kwa ada itakayokuwa imepangwa.
Maombi haya ni lazima yapitiwe na kukubaliwa na Uongozi,
kisha kupitishwa na MkutanoMkuu au Mkutano Mkuu Maalum.
ii. Baada
ya kukubaliwa Mwombaji atatakiwa kulipa Ada ya kiingilio cha kiasi
kitakachokuwa kimepangwa na Mkutano Mkuu au Mkutano Mkuu Maalum kwa wakati huo.
iii. Pamoja na Ada ya kiingilio
Mwanachama mpya atalazimika kulipa Mchango wa Miezi Miwili au zaidi Ili aweze
kuwa Mwanachama kamili wa Kikundi.
iv. Awe tayari kulipa kiingilio pamoja na ada ya uanachama ya kila mwezi
IBARA YA 13:
KUKOMA UANAKIKUNDI,
i.
Mwanakikundi akifariki.
ii.
Mwanakikundi akijiuzulu Kwa
hiari yake.
iii.
Akishindwa kuhudhuria
vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa yenye kuelezea sababu zinazoridhisha Kwa
kushindwa kwake kuhudhuria.
iv.
Akishindwa kulipa ada ya
miezi sita au Kama ana madeni sugu kwenye kikundi au miradi ya kikundi.
v.
Kufukuzwa uanakikundi
kutokana na kuthibitika kuwa.
a.
Mwakakikundi Kafanya
kazi binafsi kwa kutumia jina la kikundi bila kikundi kuwa na taarifa.
b.
Kufanya udanganyifu au
kujipatia fedha za kikundi isivyo halali.
c.
Kwa kukosa maadili na
kuvunja katiba hii pamoja na miongozo mingine ya kikundi kwa makusudi
vi.
Mwanakikundi
aliyefukuzwa Kama ilivyoelezwa hapo juu (v) hatarudishiwa fedha za ada,
kiingilio na michango ya aina nyingine isipokuwa fedha zitokanazo na miradi
aliyoshiriki kwa kadiri itakavyokuwa imeamuliwa na kikundi.
IBARA YA 14: MAJUKUMU YA
MWANAKIKUNDI YATAKUWA YAFUATAYO;
i.
Kuhudhuria vikao vyote
vya kawaida Na vya dharura.
ii.
Kushiriki katika
shughuli za wanakikundi ambazo zitaamuliwa na mkutano wa wanakikundi.
iii.
Kulipa ada ya kiingilio
na ada ya mwezi pamoja michango
mbalimbali itakayoidhinishwa na kikundi.
iv.
Kuheshimu, kusimamia na
kuzingatia katiba hii.
v.
Kuwa na nidhamu katika
mikutano, vikao na katika shughuli za Kikundi.
vi.
Kuchagua viongozi wa
kikundi kwa kadiri ya miongozi ya kikundi.
vii.
Kufuata taratibu
zilizowekwa na katiba ya kikundi au kanuni zake.
IBARA YA 15: Kurudi Kwa mwanakikundi aliyeachishwa
i.
Mwanakikundi
aliyeachishwa uanachama au kujitoa ataweza kurudi ikiwa tu itathibitika kuwa
amemaliza tatizo lililofanya uanachama wake ukome au ameomba radhi kwa kosa lililompelekea
uanachama wake kusitishwa.
ii.
Mwanachama anayeomba
kurudishwa kundini baada ya uanachama wake kusitishwa atapaswa kujaza
fomu mpya ya maombi sawa na mwananachama mpya na atatakiwa kulipa ada zote tangu tarehe ya
kuachishwa uanachama.
iii.
Muda wake wa uanachama
utatahesabiwa kuanzia aliporejeshwa kuwa mwanachama.
SEHEMU YA V: MUUNDO WA UONGOZI
IBARA YA 16:
Kikundi kitakuwa na Uongozi ufuatao
1.
Mwenyekiti.
2.
Katibu.
3.
Mwek hazina
IBARA YA 17: SIFA ZA
MWENYEKITI;
i.
Awe Na sifa zote za
mwanakikundi wa kawaida.
ii.
Awe mwanakikundi Kwa
muda wa miaka mitatu (3) mfululizo isipokuwa viongozi wa kwanza kuchaguliwa
baada ya usajili wa katiba hii hawatafungwa na sharti hili la muda.
iii.
Asiwe amepatikana Na
hatia ya kosa lolote la jinai.
IBARA YA 18: SIFA ZA
KATIBU
i.
Awe Na sifa zote za
mwanakikundi wa kawaida.
ii.
Awe mwanachama Kwa muda
wa miaka mitatu (3) mfululizo isipokuwa viongozi wa kwanza kuchaguliwa baada ya
usajili wa katiba hii hawatafungwa na sharti hili la muda.
iii.
Asiwe amepatikana na
hatia ya kosa lolote la jinai.
IBARA YA 19: SIFA ZA
MWEKA HAZINA
i.
Awe Na sifa zote za
mwanachama wa kawaida.
ii.
Awe mwanachama Kwa muda
wa miaka mitatu (2) mfululizo isipokuwa viongozi wa kwanza kuchaguliwa baada ya
usajili wa katiba hii hawatafungwa na sharti hili la muda.
iii.
Asiwe amepatikana na
hatia ya kosa lolote la jinai. iv.Awe na taaluma ya uhasibu.
SEHEMU YA V1: MAJUKUMU YA VIONGOZI
IBARA
YA 20: KAZI ZA MWENYEKITI
i.
Kuwajibika kwenye
mkutano mkuu kuhusu maswala yote ya kiutendaji ya kikundi.
ii.
Kuitisha vikao vya
Kamati Kuu na vya Mkutano mkuu kwa kufuata Kalenda ya mikutano ya Kikundi.
iii.
Kuongoza vikao na
mikutano yote ya kikundi ambayo yeye ni mjumbe.
iv.
Kusimamia utekelezaji wa
maamuzi yanayotolewa na kikundi
v.
Kutia saini katika hundi
na nyaraka mbali mbali za kitendaji kwa mujibu wa Katiba vi.Kuwa msemaji mkuu
wa kikundi.
vii.
Kuwa na kura ya turufu
katika maamuzi ambapo pande mbili zinapolingana.
viii.
Kusaini mikataba na
makubaliano kati ya kikundi na taasisi nyingine au watu binafsi kama itakavyokubaliwa
ndani ya vikao vinavyohusika ikiwa itahitajika hivyo na kanuni.
IBARA YA 21: KAZI ZA KATIBU WA KIKUNDI
i.
Kuratibu shughuli zote
za kikundi.
ii. Kukusanya taarifa za kila kikao, kutoa taarifa kwa
wanakikundi. iii. Kuweka kumbukumbu na nyaraka zote za kikundi.
iii.
Kwa kushirikiana na
Kamati Tendaji kuandaa Mikutano ya
Kikundi.
IBARA YA 22: KAZI ZA MWEKA HAZINA
i.
Kupokea fedha zote
zinazoingia katika kikundi, kuweka kumbukumbu na kuzihifadhi fedha benki au
kadiri ya maelekezo ya kamati kuu au mkutano wa kikundi.
ii.
Kutoa risiti kwa fedha
zote atakazopokea na kutunza nakala; na kupokea na kutunza stakabadhi kwa
malipo yote anayofanya.
iii.
Kuandaa taarifa za
mapato na matumizi ya kikundi kwa kila robo mwaka. iv.Kuwasilisha taarifa ya mapato na matumizi
kwenye vikao husika au itakapohitajika.
v.
Kujibu hoja za wakaguzi
wa hesabu.
vi. Kutia saini kwenye hundi. vii.Kuratibu masuala yote
yanayohusu fedha na mahesabu ya kikundi.
viii.Kutoa taarifa ya madeni ya Wanakikundi angalau
mara moja kila baada ya miezi mitatu.
SEHEMU YA VII: UCHAGUZI NA MUDA WA KUKAA MADARAKANI IBARA YA 23: MUDA WA UONGOZI
23.1
Viongozi wote katika kikundi watashika nafasi zao kwa muda wa miaka mitatu.
23.2 Kiongozi anaweza
kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili katika nafasi moja. Anaweza kuchaguliwa tena kama ameshakaa nje
ya uongozi kwa kipindi kimoja lakini anaweza kuchaguliwa katika nafasi nyingine
mara baada ya ukomo wa uongozi wake wa vipindi vya miaka mitatu.
23.3
Uchaguzi Mkuu utafanyika kila baada ya miaka mitatu. Na Kamati Kuu itaandaa kanuni
za uchaguzi.
23.4Uchaguzi mdogo unaweza kufanyika iwapo;
i.
Kiongozi au Viongozi
fulani watashindwa kuongoza kwa ajili ya kuhamishwa kikazi,
ii.
Ikiwa kiongozi atapata
ugonjwa utakaomfanya ashindwe kuendelea
na majukumu yake,
iii.
Kifo au;
iv.
kuondolewa kwa mujibu wa
katiba.
23.5.
Nafasi ya Uongozi ikiwa wazi itajazwa katika Mkutano Mkuu unaofuata
23.6.
Katika kipindi cha mpito Kamati kuu itakuwa na mamlaka ya uteuzi wa mtu miongoni
mwa wanakikundi atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi.
SEHEMU YA VIII: MIKUTANO YA KAWAIDA NA YA DHARURA
IBARA
YA 24: MKUTANO MKUU
24.1 .Mkutano
Mkuu: Kitakuwa chombo chenye maamuzi ya juu na ya mwisho katika uendeshaji wa
kikundi na shughuli zake.
24.2 .Utaongozwa
na mwenyekiti wa kikundi na kuratibiwa na katibu wake ikiwa mwenyekiti hayupo
kitaongozwa na Makamu Mwenyekiti na ikiwa Makamu Mwenyekiti hayupo, kitaongozwa
na mjumbe atakayechaguliwa na mkutano husika kuongoza mkutano mkuu huo.
24.3 .Mkutano
mkuu utaitishwa na Mwenyekiti wa kikundi
kwa kutoa notisi ya siku ishirini
na moja ikiwa ni pamoja na kuwapelekea wanakikundi agenda za mkutano huo
husika.
24.4 .Mwanakikundi anaweza
kumteua mwanakikundi mwenzake kumwakilisha kwenye mkutano mkuu (PROXY) kwa
kujaza fomu maalum au njia nyingine kadiri itakavyoamuliwa na miongozo mingine
ya kikundi. Mwanakikundi anayemwakilisha mwanakikundi mwenzake ataweza kupiga
kura kwa niaba ya mwanakikundi anayemwakilisha. Mwanakikundi hataruhusiwa
kuwakilisha zaidi ya wanakikundi wa tatu (3) katika kikao kimoja.
24.5 .Mkutano
mkuu utafanyika mara mbili kwa mwaka. Kila mkutano mkuu utapanga tarehe ya
mkutano mkuu unaofuata isipokuwa kipindi cha mkutano mkuu mmoja na mwingine
hakitazidi miezi sita (6). Kwa kuepuka mashaka mkutano mkuu wa kwanza wa
kikatiba utafanyika Jumapili. Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni wanachama wote wa
kikundi cha ASILI YETU.
24.6.Ikiwa
kwa sababu yoyote itaonekana haitawezekana
kufanyika Mkutano Mkuu katika
tarehe zilizopangwa, Kamati Kuu itakuwa na mamlaka ya kubadili tarehe ya mkutano mkuu, lakini mkutano huo
usiwe zaidi ya mwezi mmoja kabla au
baada ya tarehe iliyotajwa.
24.7. Akidi
ya mkutano mkuu ni moja ya tatu (theluthi moja) ya wanakikundi walio na
uanachama hai.
IBARA YA 25: KAMATI MBALI MBALI
25.1 KAMATI KUU
Kutakuwepo na Kamati Kuu. Itakayo
ratibu shughuli zote za kikundi Na kusimamia kamati mbalimbali. Kama hizi zita
wajibika chini ya wakuu wake
25.2. Kamati Kuu itakuwa na wajumbe wafuatao;
i.
Mwenyekiti.
ii.
Makamu wa’’
iii.
Katibu.
iv.
Katibu Msaidizi.
v.
Mweka Hazina.
vi.
Wenyeviti wa kamati
zote.
vii.
vii.Wajumbe wanne
watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu.
25.3. KAMATI YA FEDHA NA UWEKEZAJI
25.3.1 Kutakuwepo na kamati ya
Miradi. Ambayo itakuwa na wajumbe
wafuatao;
i.
Mwenyekiti
atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
ii.
Katibu atakayeteuliwa na
Kamati Kuu.
iii.
Wajumbe wanne (4)
watakaoteuliwa na Kamati Kuu.
25.4 KAMATI YA SHUGHULI ZA KIJAMII
25.4.1 Kutakuwepo na Kamati ya
Shughuli za Kijamii. Ambayo wajumbe wake
watakuwa;
i.
Mwenyekiti
atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
ii.
Katibu atakayeteuliwa na
Kamati Kuu.
iii.
Wajumbe wane
iv.
watakaoteuliwa na Kamati
Kuu.
25.5 KAMATI YA MAADILI NA MARIDHIANO
25.5.1 Kutakuwepo na kamati ya
Maadili, Nidhamu na Maridhiano ambayo
itakuwa na wajumbe wafuatao;
i.
Mwenyekiti
atakayeteuliwa na Kamati Kuu.
ii.
Katibu atakayeteuliwa na
Kamati Kuu.
iii.
Wajumbe wanne (4)
watakaoteuliwa na Kamati Kuu
25.6 KAMATI YA KATIBA NA KANUNI
25.6.1 Kutakuwepo na Kamati ya
Katiba na Kanuni ambayo itakuwa na
wajumbe wafuatao;
i.
Mwenyekiti
atakayeteuliwa Na Kamati Kuu.
ii.
Katibu atakayeteuliwa Na
Kamati Kuu.
iii.
Wajumbe wanne (4)
watakaoteuliwa Na Kamati Kuu.
25.7 KAMATI YA TEHAMA
25.7.1 Kutakuwepo Na Kamati ya
Tehama itakuwa Na wajumbe wawili watakaoteuliwa Na Kamati Kuu
IBARA
YA 26: MAJUKUMU YA KAMATI
26.0 KAZI ZA MKUTANO MKUU
26.1 Mkutano Mkuu ndio utakuwa na madaraka ya mwisho
katika kikundi.
26.2 Mkutano Mkuu utachagua viongozi wafuatao;
i.
Mwenyekiti wa Kikundi
ii.
Makamu Mwenyekiti wa
Kikundi
iii.
Katibu wa Kikundi
iv.
Katibu Msaidizi wa
Kikundi
v.
Mweka Hazina wa Kikundi
vi.
Wajumbe wanne wa Kamati
Kuu wa kikundi ambao ni, utaidhinisha uteuzi wa viongozi na wanachama wapya na
maamuzi mengine muhimu yahusuyo shughuli za kikundi.
26.3 Wajumbe waliochaguliwa katika ibara (vi) watakuwa
wajumbe wa kamati kuu pamoja na wenyeviti wa kamati.
26.4 Utapokea na kupitisha taarifa za fedha, miradi na
shughuli za kijamii za kikundi.
Kusimamia uongozi ili utekeleze maazimio ya mkutano
mkuu.
26.5 Kuamua watia sahihi wa chama kwenye mikataba
na akaunti za benki.
26.6 Kuamua na kuthibitisha wakaguzi wa nje wa hesabu
za miradi ya kikundi kadiri itakavyohitajika.
26.7 Kupokea, kujadili na hatimaye kuidhinisha mpango
kazi wa mwaka wa fedha unaoanza wa kikundi kadiri utakavyowasilishwa na kamati
kuu ya kikundi.
26.8 Kuidhinisha mkopo au vyanzo vingine vya fedha kwa
ajili ya miradi ya kikundi kadiri itakavyohitajika.
26.8.8 KAZI ZA KAMATI KUU
8.8.1 Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu
8.8.2 Kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa
na Mkutano mkuu
8.8.3 Kuwasilisha mahesabu ya fedha za kikundi kwenye
Mkutano Mkuu
8.8.4 Kuratibu shughuli na utendaji wa kikundi
8.8.5
Kujadili maombi ya wanaotaka kujiunga na kikundi na kuangalia mienendo ya
wanakikundi.
8.8.6 Kubuni mbinu za kuongeza ufanisi katika
uendeshaji.
8.8.7 Kuunda kamati ndogo na kuitisha vikao au
mikutano ya dharura pale inabopidi.
8.8.8 Kupendekeza mkaguzi wa hesabu wa Kikundi.
8.8.9 Kamati ya Kuu itakuwa na mamlaka ya kutunga kanuni na
taratibu za Kikundi na kisha
kuziwasilisha katika Mkutano Mkuu kwa
ajili ya kupitishwa. Kanuni na taratibu za utekelezaji zilizotungwa au
zitakazotungwa kuongoza shughuli
mbalimbali za kikundi hiki ni kama zifuatavyo;
i. Kanuni za kusajili wanachama wapya.
ii. Kanuni za Utendaji kazi za Uongozi.
iv.
Kanuni za Uchaguzi.
v.
Kanuni za ukusanyaji wa
udhibiti wa mali za Kikundi.
v.
Kamati ya
utendaji inaweza kupendekeza kwenye Mkutano Mkuu.
vi.
Kanuni nyingine
za utendaji wa Kikundi.
26.8.9 KAZI ZA KAMATI YA FEDHA NA UWEKEZAJI
8.9.1 Kusimamia uendeshaji
wa shughuli zote za miradi mbali mbali
ya kikundi
8.9.2 Kusimamia utekelezaji
wa sera zinazoongoza miradi
8.9.3 Kupeleka mapendekezo ya
kiutendaji kwa Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.
8.9.4 Kubuni miradi na mbinu bora za kuimarisha na kulinda
miradi.
8.9.3 Kutoa taarifa za miradi
kwenye mkutano mkuu.
8.9.4
Kuandaa utaratibu wa ajira endapo
itahitajika kuajiri wafanyakazi kwenye
miradi ya kikundi na kuufikisha
utaratibu huo mbele ya mkutano mkuu kwa
kuridhiwa.
8.9.5 Kufanya kazi nyingine
yoyote itakayopangiwa na Mkutano Mkuu.
26.9.1 KAZI ZA KAMATI YA SHUGHULI ZA KIJAMII
9.1.0 Kuratibu shughuli zote za
maafa na sherehe kuzingatia taratibu.
9.1.1 Kubuni, kupendekeza na
kuratibu mahusiano na shughuli mbalimbli kati ya kikundi na taasisi nyingine
pamoja na jamii.
26.9.2 KAZI ZA KAMATI YA MAADILI NA MARIDHIANO
9.2.1 Kupatanisha wanakikundi pale inapotokea
kutokuelewana.
9.2.2 Kupokea mashauri yote ya kinidhamu yanayohusu
mwanakikundi na kikundi ambayo yanaweza kupelekea
kusitishwa kwa uanakikundi wa mwanakikundi.
9.2.3 Kutoa taarifa ya maswala ya kinidhamu na
mahusiano kwenye kamati kuu na mkutano mkuu. Kupanga na
kuratibu maswala yanayohusu maadili na mambo ya kiroho
yanayohusu kikundi pamoja ustawi wa kikundi.
26.9.3 KAZI ZA KAMATI YA KATIBA NA KANUNI
9.3.1 Kushauri
Kamati Kuu kuhusu mambo yote ya kisheria
yanayohusika na Kikundi.
9.3.3 Kushirikiana na kamati mbalimbali katika kutengeneza kanuni za kikundi kwa kadiri ya mahitaji.
9.3.4
Kusaidia kusaidia kamati ya
maadili ikiwa kamati hiyo itahitaji
ujuzi wa kikanuni au kisheria kutoka kwa
wataalamu wa sheria.
9.3.5 Kutoa ushauri wa jumla kwa kikundi katika kuhakikisha kikundi kinatekeleza shughuli
zake kwa mujibu wa katiba yake, kanuni
na sheria za nchi.
26.9.4 KAZI ZA KAMATI YA TEHAMA
9.4.1 Kushauri Kamati Kuu kuhusu mambo yote ya
TEHAMA ambayo Kamati Kuu itahitaji
kuyafahamu katika ufanyaji maamuzi.
9.4.2 Kutoa mapendekezo mbalimbali kwa Kikundi au kamati za kikundi ya namna bora
ya kutumia TEHAMA katika kuboresha
shughuli za kikundi.
9.4.3 Kufanya kazi nyingine yoyote inayohusiana na
TEHAMA kama itakavyoagizwa na Kikundi au kamati zake.
IBARA
YA 27: MIKUTANO YA DHARURA
27.0 Wanakikundi wanaweza kuitisha Mkutano wa
dharura kujadili jambo linaloonekana kuwa la haraka na
lazima kushughulikiwa na kikundi
27.1 Ili
kuitisha mkutano wa dharura
itatakiwa wanachama wanaozidi nusu ya wanachama hai wote waweke sahihi kwenye
pendekezo lililotayarishwa na mwanachama au wanachama wanaotaka kuitisha mkutano huo wa dharura.
27.2
Baada ya wanachama zaidi ya nusu
kuweka sahihi zao kwenye pendekezo la kuitishwa kwa mkutano wa dharura, pendekezo hilo litawasilishwa kwa katibu ambaye ataanza mchakato wa kuhakikisha mkutano wa
dharura unaitishwa kama ulivyopendekeza.
SEHEMU YA IX: VIKAO NA MKUTANO
IBARA YA 28: UTARATIBU WA VIKAO NA MKUTANO
28.1 Bila kuathiri
maelezo ya ibara ya 4.1.2 ya Katiba hii, Mkutano Mkuu wa
Kikundi utafanyika kila Jumapili ya kwanza ya mwezi
Februari na kila Jumapili ya kwanza baada ya sikukuu ya Mt. Francisco.
28.2 Vikao vya
Kamati Kuu vitafanyika angalau kila baada ya miezi mitatu.
28.3 Vikao vya
Kamati za miradi na shughuli za kijamii vitafanyika angalau mara moja
kwa miezi mitatu.
28.4 Mikutano
na vikao vinaweza kufanyika zaidi pale itakapohitajika.
28.4.0 AKIDI
28.4.1 Ili
mkutano au kikao chochote kifanyike, lazima idadi ya wajumbe ifikie zaidi
ya nusu
ya wajumbe wote walio hai.
28.4.2 Kila
suala la kawaida kiutendaji litaamuliwa na wengi, mwenyekiti atakuwa na kura
ya turufu endapo itatokea kura
zinashindwa kupata uamuzi wa wengi.Maamuzi yanayohusu
kubadili ibara ya katiba hii au kumvua
mtu uanachama yatafikiwa
ikiwa tu idadi ya kura inafikia theluthi mbili ya wajumbe wote waliopiga kura.
SEHEMU YA X: UTUNZAJI WA FEDHA,VYANZO VYA FEDHA NA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIKUNDI
IBARA YA 29:MAPATO NA MATUMIZI
Mapato ya kikundi yatatokana na vyanzo vifuatavo;
i.Ada ya kiingilio kama itakavyopitishwa na mkutano mkuu.
ii.Michango
ya Ada ya kila mwezi kama itakavyokubaliwa na mkutano mkuu. iii.Faini mbalimbali kama
zitakavyopitishwa na kanuni.
iv.Faida zitokanazo na miradi
mbalimbali ya kikundi
IBARA
YA 30: VYANZO VYA FEDHA
30.1 Kutakuwa na vyanzo vya
fedha za kikundi kama ifuatavyo;
i.
Ada za kujiunga za
wanakikundi
ii.
Ada za kila mwezi za
wanakikundi
iii.
Penati mbalimbali kama
itakavyo amuliwa katika mkutano mkuu
iv.
Vyanzo vingine
vitokanavyo na riba, faida katika miradi ya kikundi
IBARA YA 31: MATUMIZI YA FEDHA
31.1
SHUGHULI ZA KIJAMII- SHEREHE
Mkutano Mkuu wa kikundi utaamua
aina ya shughuli ambazo kikundi kitahusika kwa kutoa
mchango wake kama kikundi au kwa
wanakikundi kuchangia. Maamuzi ya kikao yatadumu hadi yatakapobadilishwa na maamuzi ya kikao kingine .
31.2.
SHUGHULI ZA KIJAMII- MAAFA/ MATATIZO
Mwanakikundi, mwenzi na
wategemezi wake watastahili kuhudumiwa kama ifuatavyo;
i.
Watoto wasioidi wanne
ambao amewaainisha katika fomu
ii.
Wazazi wa mwanakikundi.
iii.
Wategemezi wasiozidi
wanne walioainishwa na mwanakikundi.
31.3UGONJWA
Mwanakikundi, mwenzi au
mtegemezi atasaidiwa kadiri ya kanuni zitakazowekwa na Kikundi.
31.4
MISIBA
Mwanakikundi akifariki, familia yake
itapewa rambirambi kutoka fedha za kikundi kama
itakavyopendekezwa na kamati kuu na kuamuliwa na mkutano mkuu. Pia
familia itapewa fedha zitokanazo na hisa
na akiba zake kwenye miradi aliyoshiriki, endapo zitakuwepo itakavyokuwa imeamuliwa na kikundi. Endapo
mwanakikundi atafiwa na mke, mtoto, mzazi au wategemezi waliotajwa katika taarifa
za mwanakikundi kwa mujibu wa kanuni za
Kikundi. Mwanakikundi atapewa rambirambi kwa
kiwango kitakachopendekzwa na
kamati kuu na kupitishwa na mkutano
mkuu.
IBARA YA 32: UENDESHAJI WA AKAUNTI ZA BENKI ZA KIKUNDI
32.0 Kwa mujibu
wa Ibara hii Kikundi kitakuwa na akaunti ya benki itakayo simamiwa na Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti, katibu na Mhazini wa Kikundi au itakavyo kuwa imeelekezwa
na Mkutano mkuu.
IBARA YA 33: TAARIFA YA FEDHA YA MWAKA
33.0 Kwa mujibu wa ibara hii taarifa
ya fedha itatolewa katika Mkutano mkuu utakao fanyika kwa
mujibu wa katiba hii. Kamati Kuu itasimamia utoaji wa ripoti za kila baada ya
Miezi mitatu
mitatu kulingana na ratiba ya vikao vya kamati hiyo kwa uongozi wa Kikundi.
IBARA YA 34: UDHIBITI NA UKAGUZI WA FEDHA
34.0 Kutakuwa na ukaguzi wa hesabu za Kikundi kama
mkutano Mkuu utakavyo kuwa umeamua.
IBARA YA 35: USIMAMIZI WA KIKUNDI
35.0 Kikundi kitakuwa na USIMAMIZI NA ULEZI wa
watu na wadau muhimu kama itavoamuliwa na Mkutano mkuu
35.1 Kikundi
kitakuwa na mlezi atakayeteuliwa na Kamati Kuu na kuthibitishwa na mkutano mkuu wa kikundi. Atakuwa ni mshauri wa
maswala yote ya kikundi.
SEHEMU YA XI: MABADILIKO YA KATIBA, MALI ZA KIKUNDI NA KUVUNJA KIKUNDI
IBARA YA 36: MABADILIKO YA KATIBA
36.1
Katiba hii inaweza kubadilishwa sehemu yake, au vipengele vyake au kuongezwa
ibara mpya au kufutwa ibara iliyopo au kuifanyia marekebisho katiba yote na
Mkutano Mkuu wa Wanakikundi kwa kura zisizopungua asilimia 75 ya wanakikundi
hai (bila PROXY) walioshiriki katika mkutano mkuu.
36.2
Mwanakikundi yeyote anayetaka kufanyia mabadiliko katiba hii au sehemu ya
katiba hii atatakiwa kutoa taarifa ya maandishi kwa katibu ambaye ataisambaza
kwa wanachama walau si chini ya miezi miwili kabla ya mkutano husika ikionyesha
aina ya mabadiliko yanayopendekezwa.
36.3 Mkutano mkuu unaweza kuyakubali
mabadiliko yanayopendekezwa au kuyafanyia maboresho mabadiliko hayo au
kuyakataa.
IBARA YA 37: MALI ZA KIKUNDI
37.1 Mali zote za Kikundi
zitakuwa chini ya jina la kikundi na zitakuwa chini ya uongozi
wa Kikundi.
37.2 Uongozi wa
kikundi utatunza kumbukumbu za mali
zinazomilikwa na kikundi kwa kadiri ya utaratibu utakaowekwa.
37.3 Mali, jina
au nembo ya kikundi vitatumika TU
kwa namna iliyoidhinishwa na
Kikundi
37.4
Mkutano mkuu wa pili wa kikundi
utachagua na kupitisha jina la Mkaguzi wa Hesabu
za kikundi. Hesabu za kikundi zitakaguliwa kila mwaka.
IBARA YA 38: KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
38.1 Kikundi hiki kinaweza kufutwa ikiwa sheria za
nchi zinalazimu kikundi kifutwe
38.2 Kikundi pia kinaweza kufutwa endapo asilimia 75
ya wanakikundi hai wataridhia hivyo katika mkutano mkuu.
38.3 Endapo kikundi kitafutwa fedha na mali zote za
miradi na uwekezaji zitatumika kwanza kulipia madeni ya kikundi yaliyopo kwa mujibu wa sheria za nchi na kulipia gharama za ufilisi na endapo kutakuwepo salio zitarudishwa kwa wanakikundi
kufuatana na uwiano wa hisa wanazomiliki.
SEHEMU YA XII: MENGINEYO
IBARA YA 39: UTATUZI WA MIGOGORO
Kwa mujibu wa ibara hii kikundi kita tumia njia ya
maridhiano ya ndani ya kikundi.
Na endapo pale mgogoro utavuka hatua hii kikundi kita
husisha walezi na wasimamizi wa kikundi.
Bila kuathiri malengo ya kikundi na kanuni zake
migogoro yote itamalizwa kwa kanuni za maadili na utendaji zitakazo kuwa
zimeundwa na Kamati Kuu kwa Mujibu wa Katiba hii.